TANGAZA NA BLOG HII KWA GHARAMA NAFUU

TANGAZA NA BLOG HII KWA GHARAMA NAFUU

Friday, 30 January 2015



Akiongea kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, hitmaker huyo wa ‘Kama Unataka Demu’, amedai kuwa baada ya kukaa kimya kwa miaka miwili ambapo alikuwa akifanya mambo ya msingi zaidi kimaisha, hivi karibuni anarejea tena kwenye muziki.


Rapper huyo amesema mashabiki wategemee mabadiliko makubwa kwakuwa muziki umebadilika na yeye hajaachwa nyuma huku akisema kuwa beat aliyoitumia kwenye wimbo huo ni kama zile zinazofanya vizuri sasa Marekani za wasanii kama ASAP Rocky au French Montana.

Amesema kwenye wimbo huo ametumia mtindo tofauti ambao watu wengi hawategemei kama anaweza kuifanya kwakuwa ni ya kizazi cha sasa.

Moe amedai kuwa amesharekodi wimbo mpya uitwao ‘Jah’ aliomshirikisha G-Nako.

Akielezea jinsi alivyorekodi wimbo huo, Moe amedai kuwa alienda kwenye studio za B Records zilizo chini ya producer Chizan Brain na kusikilizwa beat ya trap aliyoipenda.

Hata hivyo beat hiyo tayari ilikuwa imewekewa chorus aliyoifanya G-Nako iliyomvutia. Jay alimpigia G-Nako kumuomba wimbo huo uwe wake na rapper huyo wa Weusi alikubali.

Wimbo huo kwa mujibu wa Jay Moe utatoka hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment