Vuta nikuvute bungeni, Spika Makinda ahairisha Bunge
Spika wa Bunge Anna Makinda leo amelazimika kuahirisha kikao cha Bunge
kilichoanza jana, baada ya vuta nikuvute iliyotokea baada ya kutolewa
kwa hoja binafsi kutoka kwa Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha
NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuhusu jeshi la polisi kumshambulia Profesa
Ibrahimu Lipumba jana akiwa kwenye maandamano .

Spika Anna Makinda akitoa ufafanuzi Bungeni
Akizungumza katika Bunge hilo Mbatia amesema kuwa kitendo cha polisi cha
kuwapiga raia wasiokuwa na hatia, kuwazalilisha waandishi wa habari na
kupiga mabomu ya machozi kiasi cha kuwafanya watoto wadogo kuhangaika
hakikubaliki.
Amesema polisi wakiendelea kuachwa kufanya vitu vya uvunjifu wa Amani
Serikali haitatawalika hivyo ili kurejesha amani na imani ya wananchi
kwa Serikali yao ni vema shughuli zote za Bunge zikaahirishwa kupisha
mjadala wa hoja hiyo binafsi kwa lengo la kuinusuru nchi.
“Mheshimiwa Spika naliomba bunge lako liahirishe shughuli zake ili leo
tuweze kujadili suala hili la uvunjifu wa amani uliofanywa na jeshi
letu la polisi jijini Dar es Salam jana, wao wanasema kuwa wamepewa amri
kutoka ngazi za juu tunataka serikali ituambie ni nani anayetoa amri
hizi za kupiga watu wasiokuwa na hatia yeyote, amesema Mbatia.
No comments:
Post a Comment